Jumapili, 15 Machi 2015

CCM hali tete Masasi Mjini Baada ya Baba kundambanda kuchukua fomu ndani ya chama cha CUF kugombea ubunge Jimbo la Masasi Mjini

Hatimaye msanii maarufu wa vichekesho na nyimbo ambae n kipenzi cha watu wote na mkombozi wa wana wa kusini Ismail Mapembe maarufu Baba Kundambanda amechukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Masasi Mjini ndani ya Chama cha Wananchi CUF.
Akizungumza mamneno hayo kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika Nyangao alitoa salamu kwa wana CCM kuwa yuko tayari kuwakomboa wana masasi na tayari ameshachukuwa fomu. Aidha vilevile alitambulisha nyimbo yake mpya ambayo ametaja ufisadi unaofanyika katika hospitali ya Nyangao na kuwataja majina mafisadi hao. Vilevile inasemakana Masasi Hakutoshi kutokana na aliyekuwa Mbunge kupitia tiketi ya CCM baada ya kusikia kuwa Baba Kundambanda kachukua fomu yeye ameghairi kugombea tena jimbo hilo.

Jumamosi, 21 Februari 2015

Mzee Madiva wa kijiji cha Mbutta akimzungumzia Mh Bernard Kamilius Membe

Mkazi wa kijiji Cha Mbutta kata ya Mnolela Jimbo la Mtama akizungumza kwa uchungu juu ya mambo anayoyafanya Mbunge wake Mh Bernard Kamilius Membe ambaye anadhamana ya Uwaziiri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa