Kikwete: Naendelea kuimarika kila siku
japo sipo fit kabisa. Leo nazungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa,
umeenda vizuri ukiacha maeneo machache. Ni uthibibitisho wa kuendelea
na kukomaa kwa demokrasia na natoa pongezi kwa walioshinda na wakae
chini kupanga mikakati ya kuongoza maeneo yao. Katika taarifa ya waziri
Ghasia alielezea kasoro zilizojitokeza na aliahidi kuchukua hatua.
Nieleze furaha yangu kwa Hawa Ghasia juu ya hatua alizochukua na mimi
nikaweka ridhaa yangu, lazima watumishi wajue kuna adhabu ya makosa
wanayoyafanya, kuwawajibisha itakua fundisho kwao na kwa wengine wawe
makini kwenye uchaguzi wa 2015.
Jambo la pili ni sakata la Tegeta escrow, wakati wa bunge la bajeti
kulitokea madai kuwa fedha za escrow zilizokuwa benki kuu zimechotwa
kinyemela na PAP kwa kushirikiana na viongozi wa serikali. Serikali
iliahidi kutekeleza kwa kupitia kwa CAG kufanya ukaguzi ambayo ilisomwa
bungeni pia niliagiza kuchapishwa kwenye magazeti na tovuti ya
serikali, TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi wao, taarifa yao ni kuwaona
mahakamani, hawana ya maelezo. Tarehe 8 Desemba nilipoanza kazi,
niliyasoma na kutoa maagizo, zipo taarifa nilizozipata japo sio zote,
lakini nilisema siwezi kusubiri sana. Katika kusoma makaratasi na kupewa
maelekezo, yapo mambo manne mikataba ya umeme, umiliki wa PAP, kodi ya
serikali na tuhuma za rushwa.
Mikataba ya kununua umeme unaozalishwa na makampuni binafsi, mikataba ya
umeme iko ya namna mbili tozo ya umeme ikiwa ni malipo ya umeme
uliotumiwa kulingana na bei waliyokubaliana na ya pili ni gharama ya
uwekezaji(capacty charge) kwa Songas, Aggreko, IPTL
Anaelezea historia ya mgogoro wa TANESCO na IPTL, TANESCO na IPTL
walikubaliana kuanzisha akaunti ya Tegeta escrow benki kuu na kuingia
mkataba, wizara ya madini kwa niaba ya TANESCO na IPTL na benki kuu kama
wakala. Masharti ilikua kampuni ya IPTL itaendelea kupeleka madai yake
TANESCO ya tozo ya uwekezaji na TANESCO itaendelea kulipa lakini
yataenda escrow akaunti badala ya IPTL lakini ya umeme yaliendelea
kwenda IPTL na ilifunguliwa 2006 na mpaka kesi kuamuliwa 2013 wakati
IPTL inachukuliwa na PAP walikua hawajamalizana. (They decided to manage
the crisis rather than resolve it)
Kwa mujibu wa mkataba, TANESCO isipolipa inatozwa riba ya 2%, kwa mujibu
wa taarifa akaunti ilikua na 202.9 bilioni na sio 309.7, hizi zilipaswa
kuwepo endapo TANESCO ingelipa zote kwa wakati.
Fedha hizi mwenyewe nani, umma au IPTL
Nianze kuelezea ya Escrow ni kitu gani, ni tofauti kidogo na akauti zetu
tatu tulizozizoea, na akauti maalumu na kazi maalumu pia ikiisha na
yenyewe inafungwa, inasimamia na wakala na wakala pia anajukumu la
kumlipa mwenye fedha wakati ukifika.
Akaunti ikafunguliwa BoT kwa ajili ya kuweka tozo ya uwekezaji,
zinahifadhiwa ili kutoa nafasi kwa pande mbili kushughulikia tofauti zao
lakini kabla ya hapo TANESCO walikua wanalipa moja kwa moja.
Kimsingi fedha hizi ni za IPTL, katika swali pesa za nani, mdhibiti wa
hesabu alisema humu yawezekana zipo za umma pia zipo za IPTL,
Nilipomuuliza maana, akasema zamani walikua wanalipa moja kwa moja
lakini baada ya mzozo walikubaliana kwanza waziweke BoT.
Kama mgogoro ungetatuliwa na madai ya TANESCO yakakubali ya tozo
kupunguzwa, kiasi kilichopunguzwa kuna pesa za TANESCO ambazo lazima
zirudi kwa kiasi kilichopunguzwa. Bahati mbaya miaka saba baadae
halikuwa limefanyika.
Kama katika fedha hizo ipo kodi ya serikali, kwa mujibu kulikua na kodi
ya ongezeko la thamani ambayo haikulipwa, IPTL hawakuilipa na uthamini
ulikua bilioni 21 na ushee, TRA imepeleka madai yake kwa PAP.
CAG aliwaelekeza TANESCO kuacha kuhesabu pesa walizolipa kwenye akaunti
ya escrow kama pesa zao, pesa hazikufikia sifa kuhesabika kama mali ya
TANESCO(Asset). Mahakama kuu ya Tanzania ilifanya uamuzi katika shauri
la maombi ya VIP, kusimamisha mchakato wa ufilisi wa IPTL na mahakama
ikakubali.
Mfilisi aliagizwa kuhamisha kwa PAP kutoka IPTL ikiwemo akaunti escrow,
ilizua mjadala mkali. Wizara ya nishati ilimwandikia mwanasheria mkuu
kuomba ushauri, Mwanasheria akasema lipeni, uamuzi uko sawa na hauna
matatizo na benki kuu wakauliza maswali hayo hayo na majibu yakawa
yaleyale. Kuzingatia ushauri huo akaunti ikafungwa na pesa kukabidhiwa
PAP. Mjadala ukaendelea bunguni na kwenye mablogu.
Na hata TANESCO alipewa ushauri huo huo, uamuzi ule umetiliwa shaka na
kuonekana haukuwa sahihi na umeitia hasara nchi. Ukaibua hisia na ni kwa
sababu nzuri tu kwamba si bure na iko namna kama ya rushwa na watu
kunufaika binafsi. Mara kuna watu wameenda benki na kubeba pesa kwenye
sandarusi, lumbesa na mengineyo.
Jambo moja ambalo ni bahati mbaya, ilijengeka dhana kuwa akaunti
kufungwa ni jambo lililoanzishwa na maafisa wa serikali kwa manufaa yao
binafsi.
Nilipokutana na mwanasheria mkuu, alisema hakukosea katika ushauri wake na wala mahakama haikufanya makosa,
Na kuhusu ile hasara amesema hakuna hasara yyte iliyopatikana kwa sababu pesa imelipwa kwa mtu halali.
Kabla ya mzozo wa ukokotoaji TANESCO ilikuwa inailipa ITPL Moja kwa
moja. Lakini hata ulipotokea mzozo bado IPTL haikuacha kupeleka madai na
Tanesco haikuacha kulipa. Kuwepo kwa akaunti ya escrow haibadili mwenye
fedha yake.
Kwa upande wa kodi ya serikali ambazo hazikulipwa, AG alipoulizwa alisema hakuna kodi iliyochelewa kulipwa.
Mgogoro ni baina ya IPTL na TANESCO havyo uamuzi wa standard charted
haukuweza kuingia, kwa vile haikuhusishwa, ilienda kuzuia maamuzi hayo.
Fedha zilizotoka imelipwa PAP, akitokea mtu ana madai, serikali
mnaikinga vipi. Ingetokea mtu ana madai yoyote angepelekwa PAP kulingana
na makubaliano. Kukawa kuna hoja kuwa hata PAP umiliki wake wa hisa 70%
unatia mashaka kutoka Mechmar, lakini waliziuza kwanza kwa kampuni ya
Uingereza ambayo yenyewe ndo ikaziuza PAP. Kampuni ilikua chini ya
ufilisi na kwa mujibu wa taratibu huwezi kuuza ukiwa chini ya ufilisi,
kwa mujibu wa taarifa sio kweli.
Tulitaka kufanya uchunguzi sisi wenyewe na mamlaka zetu na taarifa zimeshakuja, tunazifanyia kazi.
Kuna vitu vimetokea, kuna vilivyofanyika nje na taarifa hazikuja na sasa
tunalaumiana, hivyo tunafanya uchunguzi na wote waliohusuka tunawahoji
na mahakama kuu ipo kesi ya PAP kumiliki hisa za IPTL, ipo kesi ya
uhalali wa PAP kupokea pesa za IPTL. Hatutaki kuwaingilia ila sisi
tutafanya uchunguzi wetu kwa ajili ya taarifa zetu. Tuwe na uhakika hizi
hisa zimeuzwa kwa bei gani, tunataka kujiridhisha kwa sababu ipo kodi
ya serikali(capital gain) na inalipwa na alieuza na sio alieuziwa. Kodi
hulipwa na aliepata na sio aliepoteza(Alienunua).
VIP walipouza na kupata dola milioni 78, wamelipa kodi bilioni 38.
Kulikua na tuhuma za rushwa katika mchakato mzima. Yamesemwa mengi na
bado hatujamaliza kuyasoma, rushwa ni kosa la jinai. Nilielekeza taarifa
walizozipata wazipeleke PCCB. Nimeambiwa wanaendelea na mchakato wao.
Kwa miamala, serikali inashughulika na watumishi wa umma kwa mujibu wa
taratibu, maaskofu na masheikh kupewa kitu hawatuhusu, mtumishi wa umma
ana masharti ya kupokea fedha. Watahojiwa na PCCB.
Hushtuki asubuhi akaunti ina bilioni 1.6, milioni 80 etc. Zimeanguka kutoka juu ya mti. Huo ndo utanguliza.
Maazimio ya bunge
Kwanza niseme serikali imayakubali na niwapongeze waheshimiwa
wabunge. Nashukuru kamati ya bunge chini ya Zitto na Filikunjombe, watu
wa upinzani kufanya yale maamuzi yao, kwamba CCM ni mafisadi. Ni kweli
watu hawa wanatoka CCM ila sio kwamba CCM inaridhia. Ntashangaa mbunge
kulipinga hili eti kisa tu yuko CCM, bunge wengi ni CCM, kama ni kweli
walikuwa hawataki hakuna azimio lingepita? Na kuna baadhi ya wabunge wa
CCM waliudhika na maovu haya, wenzetu wanatafuta sifa laini kwa jambo
ambalo ni letu sote.
Niwahakikishie mimi na wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira katika kutimiza maazimio ya bunge.
Kutaifisha mitambo ya IPTL, tunahimiza sekta binafsi kuwekeza,
tunapotaifisha habari tunayopeleka si nzuri, sisi tuliotaifisha mwanzo
siku hizi tunasema hatuna sera ya ujamaa hivyo waje kuwekeza. Watasema
wale jamaa wamerudia tena wanataifisha. Mahakama imefanya maamuzi kwa
IPTL, kwanza waibadili mitambo yao ibadili itumie gas badala ya mafuta,
tukiyafatilia yanaweza kutufikisha mahali. Haya ya kutaifisha yananipa
wasiwasi
Kuhusu uwazi wa mikataba na mapitio, tutafanya na lipo moja tutafanya
kuhusu usiri wao wa biashara, kuweka wazi zinaweza kutumiwa na wapinzani
wa kibiashara, hivyo tutaangalia namna ya kulifanya.
TAKUKURU na jeshi la usalama vichukue hatua, nimeshaeleza hatua zinaendelea.
Kamati za bunge kuwavua nyadhifa wenyeviti wa kamati za bunge
Raisi aunde tume ya kijaji kuwachunguza majaji(Mujulizi na Lwangisa),
nimelipokea lakini utaratibu wa kisheria kushughulikia linatakiwa
lianzie kwenye mahakama na sio linaanzia kwa rais au bunge. Mahakama
inaporidhika amepoteza sifa, inaletwa kwa rais maana ndie anaeteua
majaji. Lazima kushirikiana na muhumili wenyewe. Nilichosema tumwachie
jaji mkuu na wakiridhika watakuja kwa raisi endapo wataridhika wahusika
wamekosa sifa.
Kuhusu mabenki kuwekwa kama zinatakatisha fedha, pendekezo uchunguzi
ufanyike ni pendekezo zuri na intelligence unit ndio watakaofatilia
Serikali iandae muswada wa sheria ulioleta TAKUKURU, ni wazo zuri,
Mchakato wa kufanya mageuzi TAKUKURU tumeuanza tangu 2008. Sheria ya
kwanza ya PCCB ilikua na makosa manne tu ya rushwa tukayaongeza mpaka
24.
Kuhusu watu kuwawajibisha, bodi ya TANESCO bahati nzuri imemaliza muda
wake na tumeanza mchakato wa bodi, na tutaipata siku chache zijazo.
Katibu mkuu wa wizara ni mtumishi wa umma, hivyo kuna taratibu na nimeshaagiza zianze.
Mwanasheria mkuu wa serikali ameshajiuzulu na amesema amebeba dhamana hio pia kwa niaba ya waliojiuzulu.
Waziri wa ardhi, tumekaa nae na kuzungumza. Pesa hizi ni za nini na kwa
ajili gani na amesema ni za shule, mengi yameelezwa. Maswali makubwa kwa
nini hazijaenda shuleni moja kwa moja na zikawa kwa jina lake, akasema
ndo masharti ya mtoaji, tumelitafakari sana na tumeona msingi mkubwa wa
kimaadili kuhusu kupokea hizi pesa, tumeshazungumza nae na tumemwambia atupe nafasi tumteue mwingine.
Waziri wa nishati na madini tumemuweka kiporo, kuna uchunguzi nimeagiza
ufanywe na nikipata majibu nitafanya uamuzi, tume ya maadili pia
wanafanya kwa ajili ya kupata maamuzi kwa misingi ya haki.
NDIO MWANZO NA MWISHO WA HOTUBA YANGU NDEFU